NA MWANDISHI MAALUM, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani ulioongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Dk. Alex Gehaz Malasusa, Ikulu Jijini Dar es Salaam Leo Aprili 11,2025.
Rais Dk. Samia pamoja na viongozi hao wamejadili kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu hususani wenye changamoto ya afya ya akili.
Viongozi hao wa Kanisa wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaotoa kwa Kanisa hilo.
Aidha, kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu hususani wenye changamoto ya akili, Serikali imeahidi kushirikiana na Kanisa ili kujenga Kituo kikubwa zaidi ili watoto wengi waweze kupata huduma hiyo.