RAIS Mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha ujumbe Maalumu
wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dk. Abiy Ahmed.
Ujumbe huo umewasilishwa Ikulu jijini Addis Ababa leo April 11, 2025. Kikwete pia aliwasilisha Salamu za Rais Samia ambazo zilisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiono wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ethiopia ambao uliimarika tokea kipindi cha uanzishwaji wa Umoja wa Afrika.