NA DANSON KAIJAGE, DODOMA
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi, Joseph Mafuru amepokelewa kwa bashasha na watumishi wenzake katika Ofisi zilizopo katika mji wa Kiserikali wa Mtumba jijini hapa
Mafuru amepokelewa na Watumishi wezake huku wakimuahidi kufanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa na kwa ufanisi mkubwa.
Mapokezi hayo yamefanyika baada ya Mafuru kuteuliwa na Rais, Dk.Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa wa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.
Awali Mafuru kabla hajateuliwa na Rais Dk.Samia katika wadhifa huo, aliwahi kuwa Ofisa mipango katika Halmashauri ya Lushoto,Halmashauri ya Dodoma kabla halijawa Jiji na baadaye akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Halmashauri ya Misungwi.
Hata hivyo Mafuru amesema anamshukuru Mungu kwa kumtumia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo muhimu kwa lengo la kumsaidia katika kufanya kazi yenye tija kwa Taifa.
Sambamba na hilo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa ni lazima watumishi kufanya kazi kwa kushirikiana kwa nia ya kuweka mipango mizuri ya ardhi kwa ustawi wa mzuri wa kuondokana na matatizo yanayojitokeza katika masuala ya ardhi.