NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MSAJILI wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema Serikali ipo mbioni kuongeza mabasi 100 kwenye Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka
Mabasi hayo mapya yataenda kujikita katika njia kuu tu.
Sambamba na hilo Serikali yenye umiliki wa asilimia 85 kwenye mradi huo inakwenda kuongeza kampuni nyingine itakayosaidiana na Kampuni ya Usafirishaji ya Mabasi yaendayo Haraka(
UDART)katika utoaji huduma .
Ujio wa Kampuni hiyo itakayosaidiana na UDART utakuwa ni chachu ya kuongeza ushindani na uwajibikaji kwenye usafiri huo.
Hayo yameelezwa leo Julai 15,2024 na Mchechu alipokutana na kuzungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar es salaam kueleza kuhusu mkutano wa pili wa Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma utakaofanyika Agosti mwaka huu jijini Arusha
“Kunahitajika kampuni tatu hadi nne kwaajili ya kutoa huduma za usafirishaji kwenye mabasi ya mwendokasi ..lengo ni kutoa huduma bora…
” Uwepo wa Kampuni nyingi utasaidia kuongeza uwajibikaji lakini pia itasaidia uwepo wa huduma bora na hata ikitokea kampuni moja imegoma basi nyingine inaendelea na huduma
” Pia itasaidia kupima nani anatoa nzuri na nani ana huduma mbaya “amefafanua Mchechu
Pamoja na mambo mengine,Mchechu amerabaisha kuwa shida bado ni kubwa na mapungufu yaaonekana ndio maana, Serikali imeona ipo haja ya kuongeza kampuni nyingine kwaajili ya kutatua changamoto iliyopo
Katika hatua nyingine Mchechu amesema ili kuhakikisha hilo linafanikiwa kesho Julai 16,2024 atakuwa na kikao na benki ya NMB ambayo ndio mwezeshaji na mkopeshaji mkuu wa kununuliwa kwa mabasi hayo,
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)
na Udart kwaajili ya kukamilisha mpango huo.