NA MWANDISHI WETU, DODOMA
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) inashiriki vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) vilivyofunguliwa na Waziri wa Fedha, Dk.Mwigulu Nchemba leo Februari 7,2023 jijini Dodoma.
Timu hiyo ipo nchini kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa programu inayohusisha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta za uzalishaji.
Ujumbe wa BoT kwenye vikao hivyo unaongozwa na Naibu Gavana (Sera za Fedha na Uchumi) Dk.Yamungu Kayandabila.