NA MWANDISHI MAALUMU, BUJUMBURA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye uliopo Bujumbura nchini Burundi leo Mei 31, 2023.
Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa 21 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika nchini hapa.