NA MWANDISHI WETU, KATAVI
CHARLES Elias (18) Mkazi wa Mtaa wa Kigoma, mkoani Katavi amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu tumboni na watu wasiojulikana majira ya usiku katika eneo la Mtaa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ali Makame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa uchunguzi unaendelea.
Naye Mama wa kijana huyo aliyepoteza maisha Esther Herman ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo limesababisha kifo cha mtoto wake na kuliomba jeshi la polisi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika.
Tukio hilo linajiri ikiwa ni wiki moja imepita baada ya kutokea tukio lingine la kuuawa kwa kijana Michael Chapa mkazi wa Shanwe, kwa kile kilichodaiwa kujihusisha na vikundi vya uhalifu maarufu kama Damu Chafu