NA MWANDISHI WETU
NCHI ya Zambia inatarajiwa kuwa mweneyji wa kongamano la kwanza la wawekezaji wa Taasisi Aprili 2023.
Hayo yamebainishwa na mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa MNCapital Group yenye makao yake Afrika Kusini Michael Ndinisa kuwa Zambia imechaguliwa kuwa nchi mwenyeji kwasababu ni nchi tulivu kisiasa ambayo imeweka vivutio mbalimbali vya kukuza uwekezaji.
Ndinisa amesema jukwaa hilo linatarajiwa kufanyika kati ya Aprili 26 na 27, 2023 itakayobebwa na maada ya kuunganisha Uwekezaji Mbadala kwa Kufufua Kiuchumi
Ndinisa amesema mkutano huo wa siku mbili utawaleta pamoja wadau mbalimbali ili kujadiliana masuala yanayohusu kuchangia maendeleo endelevu ya uchumi wa Zambia na Afrika, kupitia mvuto wa uwekezaji mpya na kuongeza athari zake katika uchumi
Ndinisa amesema Jukwaa hilo ambalo ni la tatu kufanyika hadi sasa limevutia ufadhili wa Benki ya Biashara na Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), kitengo cha kifedha cha Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).
“Nchi inajivunia uchimbaji madini na usindikaji wa shaba, ujenzi, vyakula na vinywaji na mwaka 2022, uchumi wa Zambia ulikua kwa asilimia 3.1, na ipo katika nafasi ya nne kwa nchi tajiri zaidi barani Afrika kulingana na maliasili”amesema Ndinisa.
Ndinisa amesema Zambia ni kipande kibichi cha Afrika, kirafiki na chenye sehemu nyingi zenye uoto wa asili ambao hazijaharibiwa zinazostahili mwanzilishi yeyote hivyo jukwaa hilo litaongeza fursa kwa washiriki wa kongamano hilo.
“Kwa kuzingatia sifa zote zilizo hapo juu, tunafuraha na tunatarajia kuleta Jukwaa la Wawekezaji wa Kitaasisi nchini Zambia na ni Jukwaa la tatu, baada ya kufanikiwa kufika Zanzibar Februari na Namibia Machi mwaka huu”, amesema Ndinisa.
Aidha Ndinisa ameongeza kuwa Jukwaa hilo litatoa fursa kubwa kwa wawekezaji wa taasisi kufichua fursa mpya za uwekezaji na sio tu kupata faida inayotarajiwa kwenye uwekezaji, bali pia kuleta athari za kijamii.
“Washiriki katika mkutano huu watapata fursa ya kukutana na kushirikisha wadau wakuu na kukuza ushirikiano wa muda mrefu, kugundua mbinu bora zinazowasilishwa na viongozi wakuu wa fikra wa sekta hiyo”, amesema Ndinisa