NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo) leo Alhamisi, Machi 09, 2023 kitafanya mikutano ya hadhara Mkuranga na Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani.
Akizungumza na Demokrasia, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema mkutano wao wa kwanza leo utafanyika Mkuranga kuanzia saa nane mchana na wa pili utafanyika Ikwiriri-Rufiji kuanzia saa 10 jioni.
Jana tulifanya mkutano Jijini Tanga kwenye Siku ya Kimataifa ya Wanawake, sasa hivi tupo njiani tunaelekea Mkuranga na baadae Ikwiriri mkoani Pwani ambapo tutafanya mikutano ya hadhara” alisema Ado
ACT Wazalendo walizindua mikutano ya hadhara, Februari 19, 2023 Mbagala Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kuzindua mikutano Unguja na Pemba, Zanzibar.
PIA SOMA;