NA MWANDISHI WETU, NGORONGORO
MABALOZI 18 wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania wametembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kufanya utalii katika vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo
Kiongozi wa Mabalozi hao, Balozi Sandro De Olivera kutoka Nchi ya Angola ameeleza kuwa ujumbe wa mabalozi hao unajumuisha nchi za Namibia, Angola, Algeria, Msumbiji, Kenya, Somalia, Malawi, Saharawi, Namibia, Uganda, Sudan Kusini, Malawi, Nigeria na Uganda.
Balozi Olivera amebainisha kuwa wamekuwa wakisikia Utajiri wa vivutio mbalimbali vilivyoko Tanzania na kuamua kufanya Safari ya kitalii kushuhudia vivutio hivyo na kuwa Mabalozi wa vivutio hivyo wanaporudi kwenye nchi wanazoziwakilisha.
“Kuona ni Kuamini na tunaona Ngorongoro ina utajiri wa vivutio vya kila aina, ni eneo muhimu kwa mtu yoyote kutembelea na kuona” ameongeza Balozi Olivera
Naibu Kamishna wa Uhifadhi NCAA Needpeace Wambuya ameueleza ujumbe huo kuwa ujio wao ni sehemu ya kukuza mahusiano ya Kidiplomasia kupitia Sekta ya Utalii ambapo Tanzania imeendelea kutangaza vivutio vyake kwa wadau mbalimbali hali inayochangia kuendelea kupokea makundi ya wageni ikiwepo Viongozi wa mataifa mbalimbali.
Mkuu wa Huduma za Utalii NCAA Peter Makutian ameeleza ujumbe huo kuwa Ngorongoro ni eneo lenye vivutio mbalimbali ikiwemo wanyama maarufu watano (Tembo, Simba, Faru, Chui na Nyati), Kreta za aina tatu, vivutio vya malikale ambavyo ni sehemu ya urithi wa dunia, Milima na mandhari asilia yaliyohifadhiwa kwa muda mrefu