adiliyamalenga# – Demo Krasia

WANAWAKE SIKU YENU, TAMBUA TUNAWAPENDA
WANAWAKE  siku yenu, tambua tunawapenda,
Twatoka matumbo yenu, jueni tunawapenda,
Twanyonya matiti yenu, elewa tunawapenda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Twajengwa malezi yenu, msihofu twawapenda,
Na hata chakula chenu, twakipenda twawapenda,
Sasa leo siku yenu, endeleeni kupanda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Mpate elimu yenu, mbele zidisheni kwenda,
Kulea watoto wenu, jua wote wawapenda,
Kuendesha mambo yenu, mjue tunawapenda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Hebu jifanyie yenu, yale moyo unapenda,
Kama ni miradi yenu, maisha yazidi panda,
Pateni mikopo yenu, twajua mnakokwenda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Yafanyeni mambo yenu, familia zitapanda,
Bila ubunifu wenu, jua kwamba tutapinda,
Huo ni wajibu wenu, hata bila ya kupenda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Kupitia kazi zenu, na taifa litapanda,
Uchakarichaji wenu, mjue tunaupenda,
Furahieni kivyenu, jua sote twawapenda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Mwapendeza sare zenu, mwapendeza twawapenda,
Ishike nafasi yenu, nasi mzidi tupenda,
Vile ni watoto wenu, kwa malezi mwatulinda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Wengine waume zenu, kutuombea mwapenda,
Hata marafiki zenu, uwepo wetu mwapenda,
Nanyi kwa imani zenu, Mungu zidi kumpenda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Kuwapa nafasi yenu, na vile anawapenda,
Maisha ni chanzo chenu, vinginevyo tungepinda,
Twatamba uzazi wenu, dunia mnaipenda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.

Sasa hii siku yenu, tambua tunawapenda,
Ni yetu sherehe yenu, siku hii twaipenda,
Na hamko peke yenu, elewa tunawapenda,
Msalie na amani, mkijua twawapenda.
Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

MAPENZI DUNIA YAKE
MAPENZI dunia yake, tuyaache peke yake,
Tena yana bei yake, wala siashikeshike,
Mapenzi tusianike, kila mtu siri yake,
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Kila mtu ana wake, akongaye moyo wake,
Na huyo usimtake, mwenyewe akasirike,
Atokako aibuke, makubwa na yafanyike,
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Sitaki aadhirike, mwenzi wake umteke,
Pesa zako zitumike, kumfanya ageuke,
Mwenyewe yeye achoke, abaki asikitike,
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Vipi wake umtake, wako kwako asitoke?
Wa kwake anunulike, wako abaki adeke?
Kwamba yeye aumbuke, na wewe ufaidike?
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Kwa Mungu ifahamike, mabaya yasifanyike.
Amri tuzikumbuke, tena sote tuzishike.
Asijetupiga teke, na kiama tuumbuke,
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Kama mtu ana mke, halali ifahamike,
Nyumba na iheshimike, pande zote zihusike,
Wa tatu asiondoke, ya kwao yavurugike,
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Huyo ni mume wa mke, na yeye afahamike,
Wala yeye asitoke, kwingine ashike shike,
Asifanye wasumbuke, mabinti na wanawake,
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Hii na ifahamike, madhara tuyaepuke,
Mchepuko usikike, na kibano kikufike,
Wewe mochwari ufike, mwenyewe kitanzi kifike,
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Kitaka yasikufike, kwingine siyapeleke,
Huko kwako uridhike, imani yako ushike,
Maadili yatukuke, kwa waume na wake,
Kuumizana mapenzi, athari hazipimiki.

Visasi visisikike, waume dhidi ya wake,
Ncha kali zisitoke, na maisha yatoweke,
Kesi zisiongezeke, familia situkuke,
Kuumiza mapenzi, athari hazipimiki.

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

UTHUBUTU NI DARAJA
UTHUBUTU ni daraja, upate kufanikiwa,

Unakujengea hoja, kufanya yasofikiwa,

Unakwenda kama soja, sokubali kuzidiwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Una madaraja mengi, kama ukiangaliwa,

Ya kawaida ni mengi, yafanywayo na wazawa,

Ila yale ya msingi, ndiyo yanayotugawa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Kuamua kuondoka, nyumbani na kuolewa,

Huo nao kwa hakika, uthubutu unakuwa,

Kibaki mpenda mama, shida kwako kuolewa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Samaria somo kwetu, yalofanywa nao hawa,

Njaa iliota kutu, jinsi walivyowangiwa,

Wakakosa hata utu, kula waliozaliwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Wakatokea wakoma, waliokuwa wakiwa,

Wakaona njaa noma, kwa kuwafanya kulewa,

Wangeamua kugoma, kwa jinsi walivyokuwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Wenyewe wakaazimu, athari wakizijuwa,

Wakajipanga kwa zamu, kusaka vinavyoliwa,

Adui hakufahamu, akajua kavamiwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo ulipo.

Walitoka masikini, kwa mali wakajaliwa,

Na hawakuona soni, taarifa wakazigawa,

Vyakula vingi sokoni, vikauzwa kama kawa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Lazima uazimie, ya kwamba hutachachawa,

Ucheke au ulie, sikubali kuzidiwa,

Utafanya ufikie, pale utakapokuwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Katika maisha yetu, sikubali kupaliwa,

Gumu liwe kama chatu, nalo laweza kuliwa,

Fanya mambo kimtutu, utayapata maziwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Tunaendelea mbele, kwa kugoma kuzidiwa,

Hata kuwe na kelele, tunaruka kama njiwa,

Hadi tufike kilele, huku tumefanikiwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Moyo wa ajabu sana, kama vile una chawa,

Unabana zote zana, za kushinda kuvamiwa,

Ubakie kama jana, bila kitu kusifiwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Kile wewe unataka, kufanya hutalemewa,

Kama ukikitamka, na mbinu kikaundiwa,

Nakuambia hakika, utaweza kama miwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Uthubutu ndio chanzo, cha kwako kufanikiwa,

Umeshapata mafunzo, usifanye kuzuiwa,

Hebu leo iwe mwanzo, ukitaka fanikiwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Ukiwachunguza sana, kwa waliofanikiwa,

Kuthubutu kulifana, kama mechanganyikiwa,

Sasa hivi twawaona, kwamba wameshajaliwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Kuna usemi mzuri, wapaswa kusimuliwa,

Kwamba hadi kwenye dari, nako kwaweza fikiwa,

Bora mtu usikiri, kwamba umeshazidiwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Mungu akupe akili, ya furusa kuelewa,

Nawe usikae tuli, ungojee kuchangiwa,

Kwa uamuzi mkali, njiayo hutapangiwa,

Bila wewe kuthubutu, utabaki hapo hapo.

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)

lwagha@gmail.com 0767223602

WARIDHISHE NA WENZAKO
DUNIA  si yako peke, unao pia wenzako,

Ukiyarusha mateke, utaumiza wenzako,

Uwaache wasikike, kulaani mwendo wako,

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Waishi nyumba ya pango, na wapangaji wenzako,

Muziki wako ni kigongo, kuzidi hao wenzako,

Sauti yatoa nyongo, hujali hata wenzako,

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Huoni hizo kelele, ni karaha kwa wenzako?

Vipi wende wakalale, na hizo kelele zako,

Mbona maisha ya kale, si ujidunge kivyako ?

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Dunia ya kuchangia, wewe na hao wenzako,

Usijekufikiria, kwamba yote hiyo yako,

Wengine nao achia, huo uungwana wako,

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Hebu iga kwa wenzako, hawafanyi kama yako,

Wanatambua waliko, hakutaki chokochoko,

Haki za wengine huko, si za kutumbua huko,

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Kitimoto wala huko, ni haramu kwingineko,

Kwa hiyo busara iko, inajulikana huko,

Nenda ukale kiliko, usilete kwingineko,

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Una nguo nyingi zako, katika kabati lako,

Ruksa vaa kivyako, huo ni uhuru wako,

Lakini wenzako wako, za chumbani si za huko,

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Nguo kuvaa chumbani, wawavalia wenzako,

Hujui huo uhuni, wawachefua waliko?

Au hiyo yako dini, yakwambia maandiko?

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Dunia hii ni moja, ya kwetu pia ya kwako,

Ili tuishi pamoja, usitake mambo yako,

Yabakie namba moja, nyuma waweko wenzako,

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Mambo yetu jumuiya, si ya kwako peke yako,

Sawa na kuimba kwaya, huiwezi peke yako,

Sauti ni nyingi kwaya, wawepo pia wenzako,

Usidhani uko peke, waridhishe na wenzako.

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)

lwagha@gmail.com 0767223602

UBAYA WA NENO MOJA
UBAYA wa neno moja, kweli hatari jamani,
Hata ukija na hoja, vigumu kukuamini,
Wachafua kama haja, ya kuitupa shimoni,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Laweza kuwa ni Bebi, kutoka kwake mtani,
Hata kama wewe rabi, utasemwa kama nini,
Utaambiwa ni bibi, mwafanya ya kishetani,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Pengine neno mpenzi, toka mwenzako kazini,
Huyo wala sio mwenzi, kaandika kiutani,
Utayapata makonzi, ya laana mdomoni,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Anasema amepatwa, alipofika nyumbani,
Kajikuta anasutwa, kwa neno moja simuni,
Ni kwa vile ameitwa, switihati na jirani,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Hakuliki ni balaa, kama mawe kwa sahani,
Hasira zimemjaa, anakuita muhuni,
Neno moja la unaa, linaondoa amani,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Utajieleza vipi, mke kashika mpini,
Uso utaficha wapi, waonekana mgoni,
Jitetee mara ngapi, unatokoswa mekoni,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Familia huvunjika, neno likiwa kitini,
Watoto wanasumbuka, na kubaki mashakani,
Kwa sababu limetoka, neno moja mdomoni,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Muda mwingine vigumu, neno hilo libaini,
Kwamba litakuwa sumu, kwa huyo wako mwandani,
Ungejua ungedumu, kutoliweka hewani,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Ubaya wa neno moja, nani aweza baini?
Iwe wewe ni wa kuja, au mwenyeji mjini,
Lazuka kama kioja, sawa na mwiba mwilini,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Kuepuka maumivu, ni bora kutosaini,
Kwamba neno ni uovu, unaotendwa gizani,
Usisababishe povu, na kujitesa moyoni,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Kama zuia twaweza, neno lisije sokoni,
Hapo tutazipunguza, kelele nyingi nyumbani,
Upendo tutakoleza, usotutia vitani,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Ila kuaminiana, ni kuzuri kama nini,
Kwapunguza kusigana, na kukoleza amani,
Kila mtu anaona, bora heshima ya ndani,
Ubaya wa neno moja, unaleta mpasuko.

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB) lwagha@gmail.com

RUSHWA
HII bahasha ya kaki, kweli inatoa utu,
Mambo yenye unafiki, hayo yayafanya kwatu,
Kwa kuwa inabariki, yale wamejaa kutu,
Rushwa angalia rushwa, inavyopotosha haki.

Ilikuwepo zamani, na sasa wafanya watu,
Pale palipo amani, na mambo yaliyo haki,
Inacholeta uhuni, na kusababisha chuki,
Rushwa angalia rushwa, inavyopotosha haki.

Kwake Pontio Pilato, waliitumia watu,
Yuda lifanya kipato, kwa kumsaliti mtu,
Wakapita ya mkato, kwa ile yao papatu,
Rushwa angalia rushwa, inavyopotosha haki.

Alipofufuka Yesu, wakapewa rushwa watu,
Waseme yasiyohusu, kufufuka kuwe butu,
Pesa walivyoibusu, uongo ukawa kwatu,
Rushwa angalia rushwa, inavyopotosha haki.

Kutoa haki ni rushwa, wanalalamika watu,
Hata kazini ni rushwa, watu hawajali kitu,
Kwenye elimu ni rushwa, wapunjwa wana wa watu,
Rushwa angalia rushwa, inavyopotosha watu.

Michezoni nako rushwa, wanalalamika watu,
Sheria zinapindishwa, sababu ya hicho kitu,
Maamuzi kupindishwa, na kukasirisha watu,
Rushwa angalia rushwa, inavyopotosha watu.

Ni muda wa kuamshwa, kusinzia sio utu,
Tuoneshe tumechoshwa, kwa haya matendo yetu,
Tusisubiri kuoshwa, nayo TAKUKURU yetu,
Rushwa angalia Rushwa, inavyopotosha watu.

Kuweza kuendelea, tuonekane ni watu,
Bora haki pendelea, wala si rushwa ya vitu,
Uchumi tutachochea, kwa maendeleo yetu,
Rushwa angalia rushwa, inavyopotosha watu.

Hata kwa michezo yetu, ihusuyo timu zetu,
Haki iwe ndiyo yetu, kwa maendeleo yetu,
Rushwa isitajwe kwetu, kifo cha michezo yetu,
Rushwa angalia rushwa, inavyopotosha watu.

10.Kweli ipate tawala, katika matendo yetu,
Tusipende kulakula, kujaza matumbo yetu,
Hilo onyo si mkwala, latuhusu sisi watu,
Rushwa ngalia rushwa, inavyopotosha watu.

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

NATAFUTA MARAFIKI
NATAFUTA  marafiki, miongoni mwa wanangu,
Kwa mama hawabanduki, hata nikiwapa fungu,
Wanataka ipi kiki, ya kuwasogeza kwangu?
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Ada ninalipa mimi, kupitia kwa mwenzangu,
Na kitengo cha uchumi, hicho ni himaya yangu,
Iweje hawa wasomi, kwao niwe nyanya chungu?
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke

Tulipoenda likizo, mzigo likuwa kwangu,
Japo kulipia tozo, aliyefanya mwenzangu,
Na gharama zinginezo, bili yote juu yangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Wekundu wa Msimbazi, wengi wamejaa kwangu,
Japo mwenzangu mzazi, pia anayo mafungu,
Ila mengi matumizi, yako mabegani mwangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Simu zile za kisasa, kwa ajili ya wanangu,
Nilizinunua kosa, aliyewapa mwenzangu,
Mbona sasa wanitosa, na kunipiga majungu?
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Kuna wakati mwingine, wataka kampani yangu,
Nami kwa kazi zingine, ninamtuma mwenzangu,
Sasa ndio wanione, kama upepo kwa wingu?
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Niliagiza samaki, niitibu hamu yangu,
Nitafune na matoki, au chele la Usangu,
Na nyumbani sibanduki, nikisubiria changu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Samaki hawakuleta, hata wale wa mafungu,
Sebuleni wakapita, pasipo heshima yangu,
Hivi miye kwao Tata, au wa unga mzungu?
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Kuna siku nimepanga, tumtembelee Sangu,
Watoto wakaniunga, ikawa furaha yangu,
Mama yao akapinga, tutamaliza mafungu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Watoto wakageuka, safari kapigwa pingu
Ya mama yakayashika, wakayatosa ya kwangu,
Pamoja na kuumbuka, nilibaki na uchungu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Tena akafika ndugu, wa nyumbani kwa babangu,
Mke kamuona gugu, kamuwekea kiwingu,
Watoto zao vurugu, akalala kwa uvungu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Kesho yake aliaga, akiwa nje ya kwangu,
Ile simu alipiga, alisema kwa uchungu,
Na kwa kinagaubaga, kamwe hatakuja kwangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Watoto hawanitaki, wamuandama mwenzangu,
Ndugu zangu nao nduki, hawaji nyumbani kwangu,
Mbona mambo haya dhiki, kuzidi umri wangu?
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Kuwaonya nawaonya, kwani ni watoto wangu,
Mama yao kiwasonya, ndipo wanakuja kwangu,
Nikiwapa la kufanya, wadharau neno langu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Hivi niwafanye nini, wawe marafiki zangu,
Hebu nipeni maoni, mniondoe uchungu,
Hata lini hii soni, wakati nina wanangu?
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Natamani acha kazi, nikae nao wanangu,
Ndururu za matumizi, ndizo zanitia pingu,
Sipati usaidizi, kwake mzazi mwenzangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Kwenda kwa viti virefu, hiyo si tabia yangu,
Takaa muda mrefu, kuyapoteza mafungu,
Nilale kwenye sakafu, niugulie kivyangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Ni hekima toka zama, zile za wazee wangu,
Nafasi ya huyo mama, ni bora kuliko yangu,
Nabaki kushika tama, kama zee la kizungu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Watoto ona huruma, kwani nyie ni wanangu,
Pale ninapowatuma, sikiza sauti yangu,
Kama nyie mkigoma, tafupisha siku zangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Hata wewe mke wangu, nomba sinipe uchungu,
Kwa kuwateka wanangu, wasisikie ya kwangu,
Hebu umwogope Mungu, unanitia uchungu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Hii dunia ya leo, baba ninao uchungu,
Jinsi ninakosa cheo, kwa mke nao wanangu,
Nabaki kama pozeo, wakikula pesa zangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Mkituheshimu sote, mi na mzazi mwenzangu,
Mnazo baraka zote, pamoja na mali zangu,
Mtakuwa kwangu pete, kama ya huyu mwenzangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Lakini na wewe baba, yasikupate ya kwangu,
Pamoja na kunikaba, pengine sababu yangu,
Nilitenga muda haba, kuwa na watoto wangu,
Jamani nishaurini, nisibakie mpweke.

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB) lwagha@gmail.com

WATU WAMBEAWAMBEA
HILI  linawasumbua, na hata kuwaumbua,
Watu wanawatambua, na wasiowatambua,
Nguo zao wawavua, bila wao kutambua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Wewe una kitumbua, mwenyewe wakichimbua,
Uongo wanaibua, wapate kukusumbua,
Maneno wanachukua, kuyasema yanakua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Watu wanakutambua, kwa uzuri wakujua,
Wao wanayaibua, hata wasiyoyajua,
Nguo zako wakuvua, wakubutua butua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Mengine wanayajua, hata wasiyoyajua,
Ya kwao wanayajua, na watu yawazuzua,
Wamekaa kutibua, na amani kuchukua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Mchumba memuibua, kwa mipango na hatua,
Hatua mnachukua, harusi ipate kua,
Watoka usikojua, mipango wanatibua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Mpenzi bila kujua, mapya yako anajua,
Bila ya kujisumbua, ukweli kuutambua,
Pete uchumba avua, sababu huwezi jua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Kwenye ndoa twawajua, wale wanajiinua,
Amani wakiijua, wawili mnaijua,
Wanakuja kubutua, mfike msikojua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Hata kazini hutua, hili lile kuchukua,
Lengo ni kuwatibua, kwa yale yanasumbua,
Uhasama unakua, bila wenyewe kujua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Mmbea nisokujua, Mungu yeye akujua,
Watu unawasumbua na maisha kutibua,
Unadhani wachanua, Mungu meshakugundua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Ni muuaji tambua, pendo linalochanua,
Mtu ala kitumbua, kwa mchanga watibua,
Ujue umeshakua, Mungu atakuumbua,
Watu wambeawambea, ni hatari duniani.

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

SHULE ZA KATA NI ZAKE
AONDOKA  kaenda zake, zinabaki sifa zake,
Wanaume wanawake, wengi wanasema yake,
Hiyo ni alama yake, yabaki aenda zake,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Hiki umuhimu wake, acha niliseme peke,
Kwa Lowassa kazi yake, katika uhai wake,
Hili vema tutamke, kaacha alama yake,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Shule za kata ni zake, wazo lake kazi yake,
Tufurahie tucheke, watoto waelimike,
Ni vema ifahamike, Lowassa kaenda zake,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Hali ilikuwa mbaya, Kikwete wakati wake,
Shule chache angaliya, watoto watawanyike,
Wawili hawakugwaya, sekondari wasimike,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Uamuzi kila kata, iijenge shule yake,
Ni sekondari za kata, nchini tuzisimike,
Lowassa lipitapita, mtu asikengeuke,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Kwa sasa watoto wengi, hatutaki wachepuke,
Shule zimekuwa nyingi, lazima waelimike,
Tena na ajira nyingi, walimu waajirike,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Sasa wahitimu wengi, kutokea shule zake,
Wapo waupiga mwingi, kiuchumi tuibuke,
Ni kwa ule umuhimu, zile jitihada zake,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Mesoma shule ya kata, na Lowassa mkumbuke,
Jinsi alivyochakata, kwamba shule zijengeke,
Sasa ukipitapita, nyingi hata usitake,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Kitu akisimamia, ni lazima kifanyike,
Kama hujamjulia, utajua usitake,
Sasa ametangulia, mwache akapumzike,
Alifanya kazi yake,sisi twayala matunda.

Unazikwa mwili wake, na kuonekana kwake,
Walakini kazi zake, katika maisha yake,
Ni zetu siyo za kwake, zinabaki zitumike,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Sasa yamekwisha yake, na ya kwetu tuyaweke,
Kesho tuje tutajike, majina tuyasimike,
Wajao wafaidike, nasi tukaongeleke,
Alifanya kazi yake, sisi twayala matunda.

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

JAPO MGUU MMOJA
NINA mguu mmoja, mwingine umevunjika,
Kwa hatua moja moja, hivi ndivyo naondoka,
Ninajua siku moja, niendako nitafika,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Mbona hata huyo kobe, pole pole anafika,
Ni kwa nini unibebe, na wakati sijachoka,
Wewe nipigie debe, nivuke vyote vichaka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Unajua sitembei, bali ninarukaruka,
Teso langu siombei, na wewe likakufika,
Wala mimi siongei, kama nimefilisika,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Moja yangu pia bora, namshukuru Rabuka,
Nisijepigiwa kura, kwamba ninalalamika,
Mwenyewe akunje sura, na huo ajenipoka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Nitakuja piga nduru, mwisho nitakapofika,
Hata kama ni Tunduru, kelele zitasikika,
Kwamba nimeona nuru, kileleni nimefika,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Wapo wanaodhania, kwamba ninafadhaika,
Tena wanafikiria, guu moja litachoka,
Waijue yangu nia, ni kileleni kufika,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Badala ya kushangaa, na yangu kuhangaika,
Hebu cheki yako saa, muda wako wakatika,
Fanya yanayokufaa, pazuri yatakuweka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Wa mbili havai moja, msemo unasikika,
Lakini naye wa moja, anapaswa kutamka,
Kwamba anaweza kuja, hata kwa kuchoka choka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Nasema na wangu moyo, nje hayatasikika,
Usijevunjika moyo, kimoja kikikutoka,
Jua Mungu huyo huyo, hatakuacha hakika,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Miye mbele ninasonga, njiani sitadondoka,
Na mlango nitagonga, pasipo hata kuchoka,
Na maombi nitachonga, hadi nitaposikika,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Mungu wetu anajua, sisi tukihangaika,
Mizigo kwake kitua, atatupa ushirika,
Na siku tusoijua, tutakuja changamka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Ndugu sikate tamaa, yale mambo umeshika,
Hata yawe ni balaa, yanayoleta kuchoka,
Mungu atayavagaa, na yote yatayeyuka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Hata kama ni maombi, ya kuzitaka baraka,
Wewe usifanye dhambi, kwa Mungu zidi kudeka,
Kwako atapiga kambi, na kukujibu haraka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Mwenye miguu miwili, hiyo kwako ni baraka,
Situmie kikatili, wengine ukawacheka,
Yatakukuta makali, ubaki kubabaika,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Ona wale makatili, jinsi wanavyoumbuka,
Yabumbuluka madili, na kuvileta vibweka,
Mwisho wakata kauli, watupwa kwenye machaka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Ukiikosa busara, na kuuvuka mpaka,
Asoangalia sura, kifungoni takusweka,
Na huko tutakuchora, kama zile takataka,
Japo mguu mmoja niendako nitafika

Mungu wangu niongoze, njia ninayoishika,
Lengo nikalitimize, hata ipite miaka,
Wengi wakajiulize, ni kwa vipi nimefika,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Hata sasa Bwana Mungu, umenibeba hakika,
Hata kikija kiwingu, wala sitafadhaika,
Ninajua ndani yangu, katu sitajaumbuka,
Japo mguu mmoja, niendako nitafika.

Na Lwaga Mwambande
lwagha@gmail.com (KiMPAB) 0767223602